Posts

Showing posts from 2014

Busu lamtia mashakani obama

Image

YA LEO HUKO BUNGENI,RIDHIWANI KIKWETE AAPISHWA.

Image
Ilikua shangwe na furaha huko Bungeni leo,Mh.Anne Makinda akiwaapisha wabunge wapya ambao ni    Mh.Godfrey Mgimwa mbunge mpy wa jimbo la Kalenga. Mh. Mgimwa akisindikizwa kuingia katika ukumbi wa Bunge.Hakuwa peke yake,pia Mh.Spika wa Bunge alikua na kazi ya kumwaapisha Mh. Ridhiwani Kikwete kama Mbunge mpya wa jimbo la Chalinze Ukafika ule wakati wa kiapo kwa wabunge wapyaa Mh.Mgimwa akila kiapo mbele ya Spika wa bunge na wabunge huko mjini Dodoma Mh.Ridhiwani akila kiapo bungeni

Sare ya 3-3 yamliza Luis Suarez

Image
Liverpool wameona giza huku kombe la Ligi ya Premier likiwakwepa baada ya kwenda sare ya mabao matatu dhidi ya Crysral Palace . Cha kushangaza ni kwamba Liverpool walikuwa mbele kwa mabao matatu lakini Cyrstal walitifua kivumbi na kutoka nyuma bila bao huku wakimaliza mechi kwa mabao matatu sawa na Liverpool. Lakini Damien Delaney na Dwight Gayle walipunguza pengo hilo na kuingiza mabao matatu katika muda wa dakika mbili katika kipindi cha pili cha mechi.Joe Allen, Daniel Sturridge na Luis Suarez waliiweka mbele klabu yao katika muda wa saa moja kwa mabao matatu. Hali hii iliwachaa mashabiki wa Liverpool vinywa wazi wasijuie cha kusema. Liverpool sasa wako mbele ya Man City kwa poiti moja tu kwenye jedwali la alama.City bado wako na mechi moja kucheza. City watamenyana na Aston Villa katika uwanja wa Etihad mnamo siku ya Jumatano, kabla ya kumaliza msimu kwa mechi nyingine dhidi ya West Ham Jumapili.

Mourinho achukizwa matokeo ya droo

Image
Meneja wa timu ya Chelsea ya England, Jose Mourinho ameelezea kipindi cha mchezo kati ya timu yake na Norwich katika uwanja wake wa Stamford Bridge kama "kupoteza muda" katika mchezo huo uliomalizika kwa 0-0. Amewashutumu wachezaji wake kwa mchezo wa "polepole" na "uvivu" katika mchezo kabla ya kipindi cha kwanza, lakini katika kipindi cha pili ilikuwa "tofauti kabisa". Japokuwa Chelsea ilikosa nafasi ya kupaa kileleni mwa ligi kwa kuambulia pointi moja badala ya tatu ilizohitaji katika mchezo wake dhidi ya Norwich, lakini wako nafasi ya tatu na moja kwa moja kujihakikishia kucheza mashindano ya ligi ya mabingwa Ulaya, UEFA. Mpaka sasa Manchester City wanaongoza kwa pointi 80 sawa na Liverpool iliyoko nafasi ya pili zikitofautiana kwa wingi wa magoli ya kufunga. Manchester City ina magoli 59 na Liverpool ina magoli 50 baada ya zote kucheza mechi 36. Vinara hao wamebakiza mechi mbili mbili kukamilisha ligi kuu ya England msimu

Ubingwa England bado hautabiriki

Image
Manchester City imepiga hatua muhimu katika kuwania taji la ubingwa wa ligi kuu ya England wakirejea kileleni mwa ligi hiyo kwa tofauti ya magoli na Liverpool baada ya kuibwaga Everton, Jumamosi 3-2. Liverpool katika mchezo wa jana ilikuwa inawaombea majirani zao Everton kuwabwaga Manchester City, na matumaini ya kufanya hivyo yalipanda baada ya Ross Barkley kuifungia Everton bao la mapema dakika ya 11. Wachezaji wa Liverpool, Steven Gerrard na Coutinho wakishangilia moja ya magoli waliyofunga ligi kuu ya England Hata hivyo mwenye kupata ni wa kupata, City walikusanya nguvu na kupambana kikamilifu na wenyeji wao, lengo likiwa kupata pointi tatu muhimu. Sergio Aguero, ndiye aliyeanza kusafisha njia ya Manchester baada ya kutupia goli la kusawazisha katika dakika ya 22 ya mchezo na kisha kutoka nje kutokana na maumivu ya nyama za paja. Kutoka kwake kulimpa nafasi Edin Dzeko kuingia na kufunga goli lake la kwanza na la pili kwa Manchester City katika dakika ya 43. Hadi mapumziko ...

MAGEZETI YA LEO

Image

Man U yalowa kwa Sunderland

Image
Kaimu Meneja wa Manchester United Ryan Giggs amepata pigo la kwanza baada ya timu yake kupokea kichapo cha goli moja kutoka kwa Sunderland siku ya Jumamosi. Sebastian Larsson wa Sunderland ndiye aliyezima ndoto za ushindi za Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford baada ya kupachika goli zuri katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza. Sunderland ambayo ilikuwa inapigania kuepuka kushuka daraja ilionekana kutawala mchezo ambao Emanuel Giaccherini na Fabio Borin walikosa magoli baada mashuti yao kugonga mwamba. Kipindi cha pili Manchester walikuja juu na kujaribu kusawazisha goli lakini wakakosa umakini wa umaliziaji. Kwa matokeo hayo Manchester United inaendelea kubaki nafasi ya saba na pointi 60 huku Sunderland wakijihakikishia kutoshuka daraja baada ya kujikusanyia point 35 huku wakiwa wamebakiza michezo miwili.

WASANII WALIOJISHINDIA TUZO ZA KILI MUSIC AWARD

Image
Wimbo bora wa asili wenye vionjo ya Tanzania-Bora mchawi,Dar Bongo Massive 2-Msanii bora chipukizi-Young killa 3-Wimbo bora wa zouk-Yahaya,lady jaydee 4-Wimbo bora wa ragga-Chibwa ft juru -Nishai 5.Wimbo bora wa afro pop-Diamond-my no1 6.Wimbo bora wa reggae-Dabo-niwe na wewe 7.Wimbo bora wa taarab-Mzee yusuph-wasi wasi wako 8.Kikund cha mwaka cha taarab-Jahazi modern 9.Mwimbaji bora wa kike taarab-Isha Ramadhan 10.Mwimbaji bora kiume taarab-Mzee yusuph 11.Wimbo bora wa kiswahili bendi-Ushamba mzigo,Mashujaa bendi 12.Mwimbaji bora wa kiume bend-Jose Mara 13.Mwimbaji bora wakike bendi-Luiza Mbutu 14.Bendi ya mwaka-Mashujaa bendi 15.Rapa bora wa mwaka bendi-Furguson 16.Mwimbaji bora wa kike,kizazi kipya-Lady jaydee 17.Mwimbaji bora wa kiume,kizazi kipya-Diamond 18.Kikundi bora cha mwaka kizazi kipya-Weusi 19.Wimbo bora wa hiphop-nje ya box-Weusi 20.Wimbo bora wa RNB-closer-Vanesa Mdee 21.Msanii bora wa hipjop-FidQ 22.Wimbo bora wa Afrika Mashariki-Tubonge-Jose chamel...

DIAMOND ATWAA TUZO SABA ZA KILI MUSIC AWARD.

Image
Msanii wa kizazi kipya Nasib Abdul maarufu kama sukari ya mabinti diamond platinum,amejinyakulia tuzo saba mkononi,hakika diamond anastahili pongezi,pia hakuwa mbali na mlimbwende wake Wema Sepetu katika usiku wa tuzo hizo,kwani kikubwa kati ya wawili hao ni pale Wema alipomkabidhi mojawapo ya tuzo zake.......

Nigeria kufunga Shule na Ofisi Jumatano

Image
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathana ameagiza shule zote na ofisi za serikali katika mji mkuu wa Abuja nchini humo zifungwe wakati wa siku tatu za Mkutano wa Uchumi wa Dunia World Economic Forum utakaanza nchini humo jumatano ijayo. Serikali imesema hatua hiyo ni kuarahisisha misafara ya magari. Lakini suala la kuimarisha ulinzi huenda ni mambo yaliyosababisha hatua hiyo Mwandishi wa BBC Will Ross anasema akiwa Abuja. Rais Jonathan amesema polisi wapatao 5000 na wanajeshi watafanya doria na kushika hatamu za ulinzi wakati wa mkutano huo utakaoanza wiki ijayo.Ulinzi mkali umehaidiwa kwa wageni wapatao 1000 wakati wa mkutano huo. Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na Marais wa Rwanda, Senegal na Kenya ni miongoni mwa viongozi wa juu wa nchi watakaohudhuria. Mji wa Abuja katika siku arobaini zilizopita ulishambuliwa kwa matukio mawili ya mabomu yaliyoua watu wapatao tisini.

PITIA VICHWA VYA MAGEZETI LEO

Image

RAYUU ASAKA MUME......

Image
Msanii wa bongo movie ajulikanae kwa majina Alice Bagenzi alimaarufu kama Rayuu amefunguka na kudai ameshachok kuishi maisha ya ukapera,ametangaza nia yake ya kuolewa.Akifunguka na kusema;Natafuta mwaume wa kuniweka ndani awe mkweli na kunipenda kwani nimechoka maisha ya kisela,....

URAFIKI WAENDA KOMBO KATI YA WEMA NA KAJALA

Image
Ni gumzo ambalo lipo kati wa wawili hao,kwani kumeibuka fukuto la madai ya pesa tasilimu tsh.mil.13 ambazo ndo ilikua dhamana ya kajala kutoka jera ambazo zilitolewa na mrembo wema sepetu,Wema alifunguka kua anajutia kumlipia dhamana hiyo kwani imepelekea kupata matatizo tu,kwa upande wa kajala nae alifunguka hivi;yaani katika vitu wema anavyopaswa kusahau ni pamoja na iyo mil.13 aliyolipa mahakamani,simlipi ng'o,alimaliza kwa msisitizo huo.

Ni majonzi wazazi wakiandamana Nigeria

Image
Wazazi wa wasichana 230, waliotekwa nyara Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, wamefanya maandamano kuiomba serikali ya Nigeria kuongeza juhudi na kasi ya kuwatafuta watoto wao waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram. Wasichana hao walikuwa wanafunzi katika mji wa Chibok na walitekwa nyara wakijitayarisha kwa mitihani yao zaidi ya wiki mbili zilizopita. ‘‘Tunataka kuona juhudi zaidi,’’ alisema mama huyoMzazi mmoja ambaye hakutaka kutajwa , alisema kuwa wanashukuru wanigeria kwa kuwaunga mkono huku maandamano mengine yakifanyika kuwashinikiza maafisa wakuu. Kundi la wapiganaji la Boko Haram, halijasema chochote kuhusu madai kwamba wapiganaji wake ndio waliowateka nyara wasichana hao usiku wa tarehe 14 mwezi Aprili. Kundi hilo ambalo linapinga elimu ya kimagharibi , limekuwa likifanya mashambulizi Kaskazini mwa Nigeria, na inakisiwa kuwa watu 1,500 wamepoteza maisha yao mikononi mwa kundi hilo mwaka huu pekee. Mnamo siku ya Jumatano, mamia ya wanawake wa...

Ratiba kutatiza kombe la Afrika 2015

Image
Shirikisho la soka duniani FIFA limesema kuwa vilabu havitashurutishwa kuwaachilia wachezaji wao ili washiriki mechi za kufuzu kwa michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2015. Hii ni kwa sababu tarehe ya kufanyika kwa michuano hiyo iko nje ya tariba ya shirikisho hilo ya michuano ya kimataifa. Mechi za taifa bingwa Afrika, shirikisho na kombe la klabu bingwa Ulaya itafanyika kati ya tarehe 16-17.Hii huenda ikasababisha mgongano kati ya vilabu na nchi hasa ikizingatiwa mechi za ufunguzi zinazogongana na mechi za vilabu barani Afrika. Mechi hizo hazipo kwenye ratiba ya FIFA na kwa hivyo haitakuwa lazima wachezaji wa vilabu kuruhusiwa kuondoka. Hata hivyo, michuano ya makundi itakayoshirikisha Ghana, Nigeria na Cameroon, zitakuwa katika tarehe iliyoidhinishwa na FIFA , ikimaanisha kuwa vilabu vya soka kote duniani lazima viwaruhusu wachezaji wao kushiriki mechi hizo. Wachezaji kama Edward Sadomba, wataathiriwa na mgongano wa tarehe zilizo kati ya mechi za kufuzu zitakaz...

Atletico na Real Madrid katika fainali

Image
Matumaini ya Chelsea ya Uingereza kufuzu katika fainali yao ya tatu ya kombe la mabingwa barani Ulaya katika kipindi cha miaka sita iligonga mwamba uwanjani Stamford Bridge baada ya Atletico Madrid ya Uhispania kutoka nyuma bao moja kwa nunge katika kipindi cha kwanza na kuilaza the blues mabao matatu kwa moja katika mechi ya mkondo wa pili. Timu hizo zilikuwa zimetoka sare tasa katika mkondo wa kwanza huko Uhispania. Atletico walijitahidi kutafuta bao la ugenini ilikunusuru ari yao ya kuweka rekodi ya kufuzu kwenye fainali hizo na juhudi zao zilizaa matunda Adrian Lopez alipoisawazishia dakika moja kabla ya mapumziko.Vijana wa Jose Mourinho ndio walioweka bayana niya yao mapema katika mechi hii , Fernando Tores alipoiweka Chelsea kifua mbele kunako dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza . Vijana hao wa Diego Simeoni hawakulegeza kamba, kipa wao Thibaut Courtois ambaye anaichezea Madrid kwa mkopo kutoka Chelsea alifanya kazi ya ziada kumzuia John Terry na David Luiz kufunga bao . W...

Kavumbangu has signed a one year contract with the newly crowned League champions Azam

Image
Didier Kavumbagu is officially an Azam player  Goal  can exclusively reveal. Kavumbangu has signed a one year contract with the newly crowned League champions Azam and the photograph shows him wearing an Azam jersey during the signing. Kavumbagu who  Goal  had previously revealed had given Yanga two days to renew his expired contract or he will leave, has finally kept his word and signed for Azam. The Burundian striker who has scored 13 goals in the premier league this season was a free agent after his two years contract expired and had hinted to  Goal  that he had received offers from two other clubs. Kavumbagu who played two years for Yanga, signed the contract with Azam this evening, Kavumbagu joined Azam as a free agent after Yanga failed to give him a new contract. Azam team Manager Jemedar Said confirmed the signing of the player to  Goal  but didn’t disclose how much the contract or signing fee is worth. Kavumbagu finished the league secon...

Real Madrid yafuzu kwa fainali

Image
Vigogo wa ligi kuu ya Uhispania Real Madrid, wamekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kuinyeshea Mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich ya Ujerumani kwa mabao manne kwa nunge na hivyo kuibuka a ushindi mkubwa wa jumla ya mabao 5-0. Sergio Ramos alifunga mabao mawili mapema katika kipindi cha kwanza cha mechi Bao hilo lilikuwa lake la 16 katika ligi ya mabingwa barani Uropa.Kabla ya nyota wa Ureno na mchezaji bora duniani Christiano Ronaldo kuihakikishia Madrid fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 2002 na mkwaju wa wa freekick. Kwa Bayern, kichapo hicho kilikuwa ni kama wembe wa kutu kwao kwani mwaka uliopita Wajerumani hao waliifunga Barcelona 7-0 katika hatua ya nusu fainali kabla ya kuilaza Borussia Dortmund na kutwaa taji lao la tano barani ulaya. Haijulikani kufikia sasa iwapo halmashauri inayoingoza klabu hiyo itachukua hatua yeyote dhidi ya kocha wa klabu hicho Pep Guardiola ambaye licha ya kuiongoza Barca kutwaa taji la Bu...

Ronaldo avunja rekodi ya Messi

Image
Nyota wa Real Madrid ya Uhispania Cristiano Ronaldo amevunja rekodi ya Lionel Messi ya ufungaji mabao mengi zaidi katika ligi ya mabingwa barani Uropa alipoifungia timu yake mabao mawili na kuisaidia kuichapa Bayern Munich mabao 4-0 katika nusu fainali jana usiku. Kufuatia ushindi huo Real Madrid ilifuzu kwa fainali ya mchuano huo kwa jumla ya mabao 5-0.Mreno huyo mwenye umri wa miaka , 29,alifunga bao lake la 15 na 16 msimu huu katika uwanja wa Allianz Arena. Ronaldo sasa amefunga mabao 16 katika mechi kumi za ligi hiyo ya mabingwa Barani Ulaya mbili zaidi ya Lionel Messi wa Barcelona . Rekodi hiyo ya mabao 14 ilikuwa ikishikiliwa kwa pamoja kati ya Messi (2011-12, Barcelona), Ruud van Nistelrooy (2002-03, Manchester United) na Jose Altafini (1962-63, AC Milan). Kwa jumla Ronaldo amefunga mabao 67 katika ligi hiyo ya mabingwa barani ulaya sawa na Messi na ni mabao manne tu nyuma ya rekodi ya idadio kubwa zaidi ya mabao yaliyofungwa na mchezaji wa zamani wa Real na Schalke Ra...

Rais wa Brazil amuunga mkono Alves

Image
Rais wa Brazil amuunga mkono Alves kwa kula ndizi Rais Dilma Rousseff, amesifu kitendo cha mchezaji wa kimataifa wa Brazil, na Barcelona Dani Alves kutokana na tukio la ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya ligi kuu ya Uhispania, La Liga kati ya Barcelona na Villareal . Bi Rousseff aliandika katika mtandao wake wa twitter kuwa Dani Alves alionyesha ujasiri wa kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika kandanda na kuwa ni tukio la kuigwa .Mchezaji huyo wa Barcelona aliokota ndizi aliyokuwa ametupiwa na kuila kabla ya kuitupa na kuendelea na mchezo. Rais wa Brazil amuunga mkono Alves Klabu ya Villarreal inasema kuwa imempiga marufuku mwanaume ambaye alitupa ndizi hiyo uwanjani na kuwa hatohudhuria mechi zote za nyumbani za klabu hiyo maishani. Mamia ya watu na wachezaji maarufu duniani wameonyesha upendo wao kwa mchezaji huyo kwa kuweka picha zao kwenye mitandao wa kijamii wakila ndizi. Mchezaji wa Manchester City Sergio Aguero alipachika picha akila ndizi sawa na nyota ya soka y...