- Get link
- X
- Other Apps
Posts
YA LEO HUKO BUNGENI,RIDHIWANI KIKWETE AAPISHWA.
- Get link
- X
- Other Apps
Ilikua shangwe na furaha huko Bungeni leo,Mh.Anne Makinda akiwaapisha wabunge wapya ambao ni Mh.Godfrey Mgimwa mbunge mpy wa jimbo la Kalenga. Mh. Mgimwa akisindikizwa kuingia katika ukumbi wa Bunge.Hakuwa peke yake,pia Mh.Spika wa Bunge alikua na kazi ya kumwaapisha Mh. Ridhiwani Kikwete kama Mbunge mpya wa jimbo la Chalinze Ukafika ule wakati wa kiapo kwa wabunge wapyaa Mh.Mgimwa akila kiapo mbele ya Spika wa bunge na wabunge huko mjini Dodoma Mh.Ridhiwani akila kiapo bungeni
Sare ya 3-3 yamliza Luis Suarez
- Get link
- X
- Other Apps
Liverpool wameona giza huku kombe la Ligi ya Premier likiwakwepa baada ya kwenda sare ya mabao matatu dhidi ya Crysral Palace . Cha kushangaza ni kwamba Liverpool walikuwa mbele kwa mabao matatu lakini Cyrstal walitifua kivumbi na kutoka nyuma bila bao huku wakimaliza mechi kwa mabao matatu sawa na Liverpool. Lakini Damien Delaney na Dwight Gayle walipunguza pengo hilo na kuingiza mabao matatu katika muda wa dakika mbili katika kipindi cha pili cha mechi.Joe Allen, Daniel Sturridge na Luis Suarez waliiweka mbele klabu yao katika muda wa saa moja kwa mabao matatu. Hali hii iliwachaa mashabiki wa Liverpool vinywa wazi wasijuie cha kusema. Liverpool sasa wako mbele ya Man City kwa poiti moja tu kwenye jedwali la alama.City bado wako na mechi moja kucheza. City watamenyana na Aston Villa katika uwanja wa Etihad mnamo siku ya Jumatano, kabla ya kumaliza msimu kwa mechi nyingine dhidi ya West Ham Jumapili.
Mourinho achukizwa matokeo ya droo
- Get link
- X
- Other Apps
Meneja wa timu ya Chelsea ya England, Jose Mourinho ameelezea kipindi cha mchezo kati ya timu yake na Norwich katika uwanja wake wa Stamford Bridge kama "kupoteza muda" katika mchezo huo uliomalizika kwa 0-0. Amewashutumu wachezaji wake kwa mchezo wa "polepole" na "uvivu" katika mchezo kabla ya kipindi cha kwanza, lakini katika kipindi cha pili ilikuwa "tofauti kabisa". Japokuwa Chelsea ilikosa nafasi ya kupaa kileleni mwa ligi kwa kuambulia pointi moja badala ya tatu ilizohitaji katika mchezo wake dhidi ya Norwich, lakini wako nafasi ya tatu na moja kwa moja kujihakikishia kucheza mashindano ya ligi ya mabingwa Ulaya, UEFA. Mpaka sasa Manchester City wanaongoza kwa pointi 80 sawa na Liverpool iliyoko nafasi ya pili zikitofautiana kwa wingi wa magoli ya kufunga. Manchester City ina magoli 59 na Liverpool ina magoli 50 baada ya zote kucheza mechi 36. Vinara hao wamebakiza mechi mbili mbili kukamilisha ligi kuu ya England msimu
Ubingwa England bado hautabiriki
- Get link
- X
- Other Apps
Manchester City imepiga hatua muhimu katika kuwania taji la ubingwa wa ligi kuu ya England wakirejea kileleni mwa ligi hiyo kwa tofauti ya magoli na Liverpool baada ya kuibwaga Everton, Jumamosi 3-2. Liverpool katika mchezo wa jana ilikuwa inawaombea majirani zao Everton kuwabwaga Manchester City, na matumaini ya kufanya hivyo yalipanda baada ya Ross Barkley kuifungia Everton bao la mapema dakika ya 11. Wachezaji wa Liverpool, Steven Gerrard na Coutinho wakishangilia moja ya magoli waliyofunga ligi kuu ya England Hata hivyo mwenye kupata ni wa kupata, City walikusanya nguvu na kupambana kikamilifu na wenyeji wao, lengo likiwa kupata pointi tatu muhimu. Sergio Aguero, ndiye aliyeanza kusafisha njia ya Manchester baada ya kutupia goli la kusawazisha katika dakika ya 22 ya mchezo na kisha kutoka nje kutokana na maumivu ya nyama za paja. Kutoka kwake kulimpa nafasi Edin Dzeko kuingia na kufunga goli lake la kwanza na la pili kwa Manchester City katika dakika ya 43. Hadi mapumziko ...