Real Madrid yafuzu kwa fainali
Vigogo wa ligi kuu ya Uhispania Real Madrid, wamekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kuinyeshea Mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich ya Ujerumani kwa mabao manne kwa nunge na hivyo kuibuka a ushindi mkubwa wa jumla ya mabao 5-0. Sergio Ramos alifunga mabao mawili mapema katika kipindi cha kwanza cha mechi Bao hilo lilikuwa lake la 16 katika ligi ya mabingwa barani Uropa.Kabla ya nyota wa Ureno na mchezaji bora duniani Christiano Ronaldo kuihakikishia Madrid fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 2002 na mkwaju wa wa freekick. Kwa Bayern, kichapo hicho kilikuwa ni kama wembe wa kutu kwao kwani mwaka uliopita Wajerumani hao waliifunga Barcelona 7-0 katika hatua ya nusu fainali kabla ya kuilaza Borussia Dortmund na kutwaa taji lao la tano barani ulaya. Haijulikani kufikia sasa iwapo halmashauri inayoingoza klabu hiyo itachukua hatua yeyote dhidi ya kocha wa klabu hicho Pep Guardiola ambaye licha ya kuiongoza Barca kutwaa taji la Bu...