Mambo sita usiyoyafahamu kuhusu wimbo wa Msambinungwa wa Tundaman. Ni mara chache sana inatokea watu kuelewa maana ya misamiati kadhaa inayotumika sehemu tofauti mfano kwenye mashairi ya nyimbo,nahau au hata misemo kwa mfano mtu akikuuliza nini maana ya Msambinungwa unaweza kosa jibu la haraka haraka,tuitumie nafasi hii kumsikiliza Tunda Man akiuelezea wimbo huu alipoongea na millardayo.com. Swali la kwanza lilikua ni kujua maana halisi ya Neno Msambinungwa,Tundaman alijibu Msambinungwa ni mtu Fulani hivi asiyeeleweka na hafai katika jamii yaani anaweza kuwa muongo,mtu mbaya mtu mwenye vitendo visivyofaa. Swali la pili tulitaka kufahamu mpaka sasa wimbo wa Msambinungwa peke yake umemfikisha wapi kwenye hili Tundaman alijibu kwanza anamshukuru Mungu kwa mashabiki wake kwa kuipokea vizur huku akitoa mfano kuwa kuna siku moja hivi alikua anashuka kwenye gari anaenda kwa Maneck akawasikia watoto wanaimba walivyomuona wakaanza kupiga ...
MABASI YA MWAKYEMBE YAANZA KUTESA APA MUJINI BONGO LIVE!! Mmoja ya basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatizo la usafiri katika jiji la Dar.
Picha za kikao cha NEC-CCM leo Jumapili Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili ukumbini kuendesha Kikao Maalum Cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, mjini Dodoma leo, Feb 16, 2014. Wajumbe wa NEC, na Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakiwa ukumbini. Kushoto ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro. Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, leo Feb 26, 2014. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk. Sheni Sekretarieti ya Kikao Cha NEC ikiwa tayari kwa kazi ukumbini leo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) akimsikiliza kwa Mzee Kazidi kutoka Kilimanjaro, wakati wakijadili ja...
Comments
Post a Comment